Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo
Awesome Image

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea na mchakato wa utafiti, utafutaji na uchimbaji wa mauta na gesi hasa katika ameneo ya bahari Zanzibar. Lakini, licha ya kuwepo kwa taasisi maalumu zinazohusika na utafutaji wa mkondo wa juu wa Mafuta na Gesi Asilia bado kuna changamoto mbali mbali katika kuharakisha upatikanaji wa matunda ya Sekta hii. Ndio maana Serikali kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi itaendelea kuhakikisha uwepo wa usimamizi bora wa shughuli za mafuta na gesi asilia na kuongeza uwezo wa taasisi zilizopo zinazoshughulikia udhibiti na utafutaji wa mafuta na gesi asilia, ikiwa ni pamoja na kuiongezea Kampuni ya Mafuta ya Zanzibar jukumu la kufanya biashara ya mafuta na gesi asilia kwa mkondo wa chini.

Vipaumbele vya Sekta hii ya Mafuta na Gesi ni pamoja na:

• Kuongeza uwezo wa kitaasisi katika kusimamia na kukuza sekta ya mafuta na gesi asilia.
• Kuipatia Kampuni ya Mafuta ya Zanzibar jukumu la kufanya biashara ya mafuta na gesi asilia kwa              mkondo wa chini.
• Kuimarisha uwezo wa taasisi za mafuta na gesi asilia kwa kufanya marekebisho ya kisera na kisheria.
• Kuandaa mikakati ya mawasiliano bora juu ya maendeleo ya utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi             asilia.
• Kufanya na kusambaza tafiti za kimkakati za tathmini ya athari za Mazingira zinazohusu maendeleo ya    mafuta na gesi asilia.
• Kuendeleza mchakato wa mashauriano na jamii kuhusu maendeleo ya mafuta na gesi asilia.
• Kujenga uwezo wa kiutendaji na mbinu za uwezeshaji kwa ajili ya kuwanufaisha wazawa.
• Kutenga eneo lililo salama kwa ajili ya ujenzi wa Hifadhi ya Taifa ya Takwimu za mafuta na gesi asilia.
• Kujenga uwezo wa usalama na uhifadhi wa takwimu kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Takwimu za mafuta    na gesi asilia.
• Kuanzisha taasisi mahiri yenye mfumo imara utakaohakikisha usimamizi bora wa mapato ya mafuta na    gesi asilia.
• Kuanzisha mfumo wenye uwazi wa ukusanyaji wa mapato ukaosimamia maamuzi na matumizi ya             mapato ya mafuta na gesi asilia kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi
• Kuunda programu za uhamasishaji wa umma juu ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi asilia.

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.