Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo
  • Dhamira Yetu

    Kuimarisha usimamizi na matumizi endelevu ya rasilmali za baharí kupitia fursa mbali mbali za uwekezaji katika uchumi wa buluu, ujasiriamali pamoja na uwezeshaji wa wananchi, na kuhakikisha haki na maslahi ya jamii katika fursa hizo.

  • Dira Yetu

    Kuigeuza Zanzibar kuwa kitovu cha maendeleo ya Uchumi wa Buluu katika Eneo la Magharibi ya Bahari ya Hindi.

  • Malengo Yetu

    • Kusimamia maendeleo endelevu ya sekta ya Uvuvi na Mazao ya Baharini.
    • Kusaidia na kushajiisha fursa mbali mbali za ubia baina ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi katika Uchumi wa Buluu.
    • Kutekeleza malengo ya uwezeshaji wa waajasiriamali na wananchi kwa ujumla katika Uchumi wa Buluu.
    • Kusimamia utafutaji na uchimbaji wa rasilmali ya mafuta na gesi.
    • Kuendelea na juhudi za utafiti na uwezo katika kutafuta fursa mbali mbali za nishati mbadala.
    • Kupambana na uharibifu na uchafuzi wa mazingira ya baharí na kusimamia hifadhi za maeneo ya baharí.
    • Kusimamia na kuendeleza utafiti wa sekta ya uvuvi na rasimali za baharí
    • Kuongeza mashirikiano na sekta mbali mbali katika uratibu wa masuala ya diplomasia ya uchumi wa buluu, usimamizi wa baharí na usalama wa baharí,

  • Tunu Zeetu

    • Uwazi.
    • Kujitolea
    • Ubunifu
    • Ubora
    • Umoja
    • Mashirikiano

  • Vipaumbele Vyetu

    • Uwezeshaji na Uwekezaji katika Uvuvi Endelevu wa Mwambao na Bahari Kuu
    • Uwezeshaji na Uwekezaji katika Kilimo cha Mwani
    • Uwezeshaji na Uwekezaji katika Ufugaji wa Viumbe Maji (Matango Bahari, Kaa, Samaki)
    • Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi
    • Nishati Mbadala ya Baharini
    • Ujenzi wa Miundo Mbinu ya Bandari, Masoko, Viwanda, Huduma na Biashara za Uchumi wa Buluu
    • Utafiti wa Uvuvi, Bahari, Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi Baharini
    • Uhifadhi wa Maeneo ya Bahari (Matumbawe, Nyasi Bahari, Mikoko na Bioanuwai ya Baharini)
    • Utalii Endelevu wa Bahari
    • Usimamizi wa Bahari (Usalama wa Bahari, Kuimarisha Ulinzi wa Bahari na Kupambana na Uvuvi Haramu Usioripotiwa)

  • Huduma Zetu

    • Utoaji wa leseni na vibali vya Uvuvi
    • Utoaji wa leseni na vibali ya mazao ya baharini
    • Utoaji wa vibali vya usafirishaji wa bidhaa za mazao ya baharini nje ya nchi.
    • Usimamizi wa uingiaji na utozaji wa ada kwa watalii ndani ya hifadhi za baharí.
    • Uboreshaji wa viwango vya mazao ya uvuvi, mwani na mazao ya baharini.
    • Usimamizi wa leseni za utafutaji wa mafuta na gesi.

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.