Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar (Zanzibar Fisheries Research and Marine Resource Institute) – ZAFIRI, ni Taasisi mpya iliyoanzishwa tarehe 23 April, 2019 kwa Hati ya Sheria (Legal Notice) Nambari 32, chini ya kifungu 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kifungu 55 cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Act Nam. 2 ya mwaka 2011 kwa madhumuni ya kuendeleza tafiti za Uvuvi na Maliasili za baharini Zanzibar ili kuimarisha sekta ya Uvuvi, ukulima wa mazao ya baharini na uhifadhi wa mazingira ya Bahari nchini.

Mkurugenzi Mkuu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini atakua ni mtendaji na msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za Taasisi. Mkurugenzi Mkuu anaeteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa kifungu Na. 24 (1) cha Hati ya Sheria nambari 32 ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar.

Dira
Kuwa kituo bora cha utafiti wa uvuvi, maliasili za baharini na sayansi za bahari katika eneo la ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi.
Dhamira
Kufanya tafiti za kisasa za uvuvi, rasilimali za bahari na sayansi za bahari, pamoja na kuendeleza mbinu na ubunifu bora ili kutoa muongozo wa matumizi endelevu ya rasilimali za bahari, maendeleo ya sekta za uvuvi na ukulima wa mazao ya baharini, na uhifadhi wa mazingira ya bahari.
Majukumu
Kwa mujibu wa Hati ya Sheria inayounda Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini ya mwaka 2019, kifungu namba 6(1) kimeipa mamlaka taasisi hii kuwa na majukumu yafuatayo:
a. Kuratibu na kusimamia shughuli zote za utafiti wa Uvuvi na maliasili za baharini ndani ya Zanzibar.
b. Kufanya tafiti za uvuvi na maliasili za baharini katika eneo la maji ya ndani ya nchi, na maji ya ukanda wa kiuchumi wa Bahari.
c. Kuendeleza na kukuza mbinu bora, tekinolojia na ubunifu katika sekta za uvuvi, ufugaji na usarifu wa Samaki na mazao ya baharini.
d. Kuanzisha na kuendeleza udhibiti wa ubora wa bidhaa za Samaki na raslimali za bahari, uhifadhi wa rasilimali baada ya mavuno na ubunifu wa teknolojia bora katika mnyororo wa thamani wa samaki na rasilimali za Bahari.
e. Kukuza na kushajihisha njia za kisayansi za uhifadhi wa rasilimali za bahari na mifumo wa ikolojia ya Bahari.
f. Kuelimisha na kutoa mrejesho wa matokeo ya utafiti kupitia majarida, miongozo, nyaraka za tafiti, machapisho mengine na majukwaa yanayohusiana na tafiti za rasilimili za bahari pamoja na kuendeleza kazi za Taasisi.
g. Kupendekeza mfumo ambao utajumuisha shughuli za utafiti wa uvuvi, rasilimali za bahari na sayansi bahari kwa ajili ya Taasisi za umma na zisizo za kiserikali pamoja na watu wanaohusika katika tasnia ya uvuvi nchini.
h. Kuboresha matumizi ya teknolojia kwa ajili ya ufugaji wa samaki na rasilimali za Bahari.
i. Kuzitafuta, kuzihifadhi na kutoa mrejesho wa taarifa za kisayansi na teknolojia zinazohusiana na uvuvi na rasilimali za Bahari.
j. Kuanzisha na kutunza kituo cha kuhifadhi nyaraka na taarifa za uvuvi na rasilimali za baharini.
k. Kushirikiana na taasisi za kitaifa, kikanda, kimataifana wadau wanaofanya tafiti za uvuvi na rasilimali za Bahari.

Idara
Taasisi itakuwa na Idara nne (4) zifuatazo:
1) Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango
2) Idara ya Utafiti, Ubunifu na Uelimishaji
3) Idara ya Maabara
4) Ofisi ya Uratibu Pemba

Divisheni
Taasisi itakuwa na Divisheni kumi (10) ambazo zitaongozwa na Wakuu wa Divisheni kwa mujibu wa muundo wa utumishi na wataripoti moja kwa moja kwa Wakurugenzi wa Idara kwa mujibu wa muundo wa Idara husika.

Divisheni hizo ni kama zifuatazo:
1) Divisheni ya Utawala na Rasilimaliwatu
2) Divisheni ya Mipango..
3) Divisheni ya Utunzaji Kumbukumbu .
4) Divisheni ya Utafiti wa Uvuvi na Ukulima/Ufugaji wa Viumbe vya Baharini .
5) Divisheni ya Utafiti wa Uhifadhi na Mazingira ya Bahari.
6) Divisheni ya Ubunifu na Uelimishaji.
7) Divisheni ya Maabara ya Kemia.
8) Divisheni ya Maabara ya Biolojia.
9) Divisheni ya Maabara ya Uzalishaji wa Viumbe vya Baharini.
10) Divisheni ya Maabara ya Mifumo ya Bahari.

Vitengo
Aidha, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar itakuwa na vitengo sita (6) vitakavyoongozwa na Wakuu wa Vitengo kwa mujibu wa muundo wa utumishi na vitakuwa vinaripoti moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu,vitengo hivyo ni kama vifuatavyo:
1) Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
2) Kitengo cha Ununuzi na Uondoshaji Mali
3) Kitengo cha Uhasibu
4) Kitengo cha Huduma za Sheria
5) Kitengo cha Uhusiano wa Umma
6) Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Takwimu
Maelezo zaidi

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.