Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo

Idara hii inahusika na shughuli za kusimamia, kuendeleza na kushirikisha jamii katika Uhifadhi wa Maeneo ya Bahari. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Majukumu ya Idara ya Uhifadhi wa Maeneo ya Bahari ni pamoja na:
• Kusimamia na kuendeleza maeneo ya hifadhi za bahari.
• Kuanzisha maeneo mapya ya hifadhi za bahari.
• Kushirikisha jamii katika Uhifadhi wa maeneo ya bahari.
• Kufanya tathmini mbali mbali za uendelezaji na Uhifadhi wa maeneo ya bahari.
• Kutoa uelewa kwa jamii kuhusu Uhifadhi wa bahari na fursa zake za kiuchumi.
• Kusimamia Doria katika maeneo ya hifadhi za bahari.
• Kuendeleza maeneo ya urithi yaliyo ndani ya maeneo ya hifadhi za bahari.

Idara ya Uhifadhi wa Maeneo ya Bahari itaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni:-
1. Divisheni ya Uhifadhi wa mazingira ya bahari, bio-anuwai na rasilimali bahari.
Divisheni hii inahusika na kusimamia na kutekeleza mipango ya uhifadhi wa viumbe bahari kama vile mikoko, majani bahari, matumbawe yenye umuhimu wa malisho na kwa ukuwaji wa viumbe vyengine vya baharini pamoja na kuainisha maeneo maalum yenye umuhimu kwa uhifadhi wa rasilimali za bahari.

2. Divisheni ya Uhifadhi shirikishi na maendeleo ya jamii
Divisheni hii inahusika na kutoa mafunzo ya uvuvi, shughuli mbadala za kiuchumi na uhifadhi kwa jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi na wadau mbali mbali wa uhifadhi wa bahari pamoja kufanya jitihada za kuwafikia waliombali (outreach) kuhusiana na mambo mbali mbali yanahusiana na uhifadhi wa maeneo ya bahari.

3. Divisheni ya ulinzi na usimamizi wa sheria (doria).
Divisheni hii inahusika na kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo mbali mbali juu ya uvuvi, utalii na shughuli nyengine kwenye maeneo ya hifadhi na kuendesha doria katika maeneo yote ya hifadhi.

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.