Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo

Idara hii inahusika na kudhibiti na kuendeleza shughuli za uvuvi endelevu, kilimo cha mwani, na ufugaji wa viumbe maji kama vile Matango Bahari, Kaa Tope, na Samaki. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Majukumu ya Idara ya Maendeleo ya Uvuvi ni pamoja na:

• Kusimamia, kukuza, kuendeleza, kudhibiti na kufuatilia shughuli za uvuvi endelevu, kilimo cha mwani, na ufugaji wa viumbe maji.
• Kusimamia tathmini mabli mbali za maendeleo ya shughuli za uvuvi na mazao ya baharini.
• Kusimamia na kutekeleza mipango ya utekelezaji wa program za uvuvi na mazao ya baharini ikiwemo takwimu, elimu, nyenzo, miundo mbinu, viwanda, mitaji na masoko.
• Kusimamia ukusanyaji wa tozo na takwimu za uvuvi na mazao ya baharini
• Kuinua uelewa wa jamii juu ya umuhimu wa uvuvi endelevu, miundombinu, zana bora, mitaji na masoko.
• Kusimamia utekelezaji wa sheria na kanuni za uvuvi endelevu.

Idara ya Maendeleo ya Uvuvi inaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni:-
1. Divisheni ya Uvuvi.
Divisheni hii inahusika na kuwawezesha na kuwajengea uwezo wavuvi wadogo kwa ajili ya kuimarisha Shughuli za Uvuvi nchini.

2. Divisheni ya Ufugaji wa Viumbe vya Baharini
Divisheni hii inahusika na kusimamia na kuratibu shughuli za ufugaji wa Viumbe vya Baharini pamoja na kuanzisha mashamba ya mfano kwa kushirikiana na jamii katika ukuzaji wa sekta ya Uvuvi.

3. Divisheni ya Usarifu wa Mazao ya Baharini.
Divisheni hii inahusika na kuratibu shughuli za usarifu na ukuzaji masoko kwa mazao ya Baharini.

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.