Karibu Katika Tovuti ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar

STAFF MAIL : Login

Awesome Logo

Idara ya Mipango Sera na Utafiti ina jukumu la Kuandaa na Kusimamia Utekelezaji wa Sera, Sheria na Mipango ya Wizara. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Majukumu ya Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ni pamoja na:
• Kuandaa na kufanya mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni za Wizara.
• Kusimamia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za Wizara.
• Kusimamia utekelezaji wa Matamko/Maagizo/Mapendekezo ya Serikali pamoja na kuandaa nyaraka muhimu za Serikali.
• Kusimamia uandaaji wa Mipango na Bajeti ya Wizara kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi.
• Kubuni na kuandaa Mapendekezo ya Miradi ya Maendeleo kwa Wizara.
• Kuandaa viashiria vya matokeo ya utekelezaji wa Mipango ya maendeleo ya Sekta ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi.
• Kutoa uelewa kwa umma kuhusu Sera, Sheria, Mipango na Mikakati mbalimbali inayousiana na maendeleo ya Sekta ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi.
• Kuratibu shughuli mtambuka katika sekta ya uchumi buluu na uvuvi.

Idara hii inaundwa na Divisheni Kuu nne (4) ambazoni:-
1. Divisheni ya Maendeleo ya Sera.
Divisheni hii inahusika na shughuli za kuandaa, kusimamia nakufuatilia utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za Sekta ya Uchumi Buluu na Uvuvi.

2. Divisheni ya Mipango ya Kisekta na Maendeleo
Divisheni hii inahusika kuandaa na kusimamia utekelezaji Mipango na Bajeti ya Wizara.

3. Divisheni ya Ufuatiliaji na Tathmini.
Divisheni hii inahusika na kufuatilia na kufanya tathimini ya utekelezaji wa mipango ya Wizara.

4. Divisheni ya Utafiti.
Divisheni hii inahusika na kuratibu tafiti na takwimu kwa Sekta ya Uchumi Buluu na Uvuvi.

Choose Your Color
You can easily change and switch the colors.