UHIFADHI NA MAENEO YA BAHARINI
Idara hii inahusika na shughuli za kusimamia, kuendeleza na kushirikisha jamii katika Uhifadhi wa Maeneo ya Bahari. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Dr. Makame Omar Makame
Mkurugenzi Idara ya Uhifadhi na Maeneo ya Baharini
Idara ya Uhifadhi wa Maeneo ya Bahari itaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni:
Divisheni hii inahusika na kusimamia na kutekeleza mipango ya uhifadhi wa viumbe bahari kama vile mikoko, majani bahari, matumbawe yenye umuhimu wa malisho na kwa ukuwaji wa viumbe vyengine vya baharini pamoja na kuainisha maeneo maalum yenye umuhimu kwa uhifadhi wa rasilimali za bahari
Divisheni hii inahusika na kutoa mafunzo ya uvuvi, shughuli mbadala za kiuchumi na uhifadhi kwa jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi na wadau mbali mbali wa uhifadhi wa bahari pamoja kufanya jitihada za kuwafikia waliombali (outreach) kuhusiana na mambo mbali mbali yanahusiana na uhifadhi wa maeneo ya bahari
Divisheni hii inahusika na kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo mbali mbali juu ya uvuvi, utalii na shughuli nyengine kwenye maeneo ya hifadhi na kuendesha doria katika maeneo yote ya hifadhi



