Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar

  • Mwanzo
  • Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar

ZAFIRI

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar (Zanzibar Fisheries Research and Marine Resource Institute) – ZAFIRI, ni Taasisi mpya iliyoanzishwa tarehe 23 April, 2019 kwa Hati ya Sheria (Legal Notice) Nambari 32, chini ya kifungu 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kifungu 55 cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Act Nam. 2 ya mwaka 2011 kwa madhumuni ya kuendeleza tafiti za Uvuvi na Maliasili za baharini Zanzibar ili kuimarisha sekta ya Uvuvi, ukulima wa mazao ya baharini na uhifadhi wa mazingira ya Bahari nchini.

Dr. Zakaria Ali Khamis
Mkurugenzi mkuu ZAFIRI

MKURUGENZI MKUU

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini atakua ni mtendaji na msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za Taasisi. Mkurugenzi Mkuu anaeteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa kifungu Na. 24 (1) cha Hati ya Sheria nambari 32 ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar.

DIRA

Kuwa kituo bora cha utafiti wa uvuvi, maliasili za baharini na sayansi za bahari katika eneo la ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi.

DHAMIRA

Kufanya tafiti za kisasa za uvuvi, rasilimali za bahari na sayansi za bahari, pamoja na kuendeleza mbinu na ubunifu bora ili kutoa muongozo wa matumizi endelevu ya rasilimali za bahari, maendeleo ya sekta za uvuvi na ukulima wa mazao ya baharini, na uhifadhi wa mazingira ya bahari.

MAJUKUMU

Kwa mujibu wa Hati ya Sheria inayounda Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini ya mwaka 2019, kifungu namba 6(1) kimeipa mamlaka taasisi hii kuwa na majukumu yafuatayo:

Kuratibu na kusimamia shughuli zote za utafiti wa Uvuvi na maliasili za baharini ndani ya Zanzibar
Kufanya tafiti za uvuvi na maliasili za baharini katika eneo la maji ya ndani ya nchi, na maji ya ukanda wa kiuchumi wa Bahari
Kuendeleza na kukuza mbinu bora, tekinolojia na ubunifu katika sekta za uvuvi, ufugaji na usarifu wa Samaki na mazao ya baharini
Kuanzisha na kuendeleza udhibiti wa ubora wa bidhaa za Samaki na raslimali za bahari, uhifadhi wa rasilimali baada ya mavuno na ubunifu wa teknolojia bora katika mnyororo wa thamani wa samaki na rasilimali za Bahari
Kukuza na kushajihisha njia za kisayansi za uhifadhi wa rasilimali za bahari na mifumo wa ikolojia ya Bahari
Kuelimisha na kutoa mrejesho wa matokeo ya utafiti kupitia majarida, miongozo, nyaraka za tafiti, machapisho mengine na majukwaa yanayohusiana na tafiti za rasilimili za bahari pamoja na kuendeleza kazi za Taasisi
Kupendekeza mfumo ambao utajumuisha shughuli za utafiti wa uvuvi, rasilimali za bahari na sayansi bahari kwa ajili ya Taasisi za umma na zisizo za kiserikali pamoja na watu wanaohusika katika tasnia ya uvuvi nchini
Kuboresha matumizi ya teknolojia kwa ajili ya ufugaji wa samaki na rasilimali za Bahari
Kuzitafuta, kuzihifadhi na kutoa mrejesho wa taarifa za kisayansi na teknolojia zinazohusiana na uvuvi na rasilimali za Bahari
Kuanzisha na kutunza kituo cha kuhifadhi nyaraka na taarifa za uvuvi na rasilimali za baharini
Kushirikiana na taasisi za kitaifa, kikanda, kimataifana wadau wanaofanya tafiti za uvuvi na rasilimali za Bahari
IDARA

Taasisi itakuwa na Idara nne (4) zifuatazo:

Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango
Idara ya Utafiti, Ubunifu na Uelimishaji
Idara ya Maabara
Ofisi ya Uratibu Pemba
DIVISHENI

Taasisi itakuwa na Divisheni kumi (10) ambazo zitaongozwa na Wakuu wa Divisheni kwa mujibu wa muundo wa utumishi na wataripoti moja kwa moja kwa Wakurugenzi wa Idara kwa mujibu wa muundo wa Idara husika.

Divisheni hizo ni kama zifuatazo:

Divisheni ya Utawala na Rasilimaliwatu
Divisheni ya Mipango
Divisheni ya Utunzaji Kumbukumbu
Divisheni ya Utafiti wa Uvuvi na Ukulima/Ufugaji wa Viumbe vya Baharini
Divisheni ya Utafiti wa Uhifadhi na Mazingira ya Bahari
Divisheni ya Ubunifu na Uelimishaji
Divisheni ya Maabara ya Kemia
Divisheni ya Maabara ya Biolojia
Divisheni ya Maabara ya Uzalishaji wa Viumbe vya Baharini
Divisheni ya Maabara ya Mifumo ya Bahari
VITENGO

Aidha, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar itakuwa na vitengo sita (6) vitakavyoongozwa na Wakuu wa Vitengo kwa mujibu wa muundo wa utumishi na vitakuwa vinaripoti moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu,vitengo hivyo ni kama vifuatavyo:

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Kitengo cha Ununuzi na Uondoshaji Mali
Kitengo cha Uhasibu
Kitengo cha Huduma za Sheria
Kitengo cha Uhusiano wa Umma
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Takwimu

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.

Melbourne, Australia
(Sat - Thursday)
(10am - 05 pm)
Shopping Cart (0 items)
Translate »