UTALII ENDELEVU
Utalii wetu wa Zanzibar ni utalii wa bahari. Ni utalii unaotegemea uhai na afya ya bahari na rasilmali zake. Hivyo Utalii Endelevu ni ule unaojali hifadhi za maeneo ya bahari, bioanuwai ya bahari, usafi na mazingira safi ya fukwe na bahari zake. Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi inapigania sana Utalii Endelevu wa Zanzibar unaojali mazingira ya bahari pamoja na mila na desturi za watu wa Zanzibar.
Serikali itahakikisha uhifadhi wa mila, desturi na tamaduni za nchi, chini za kaulimbiu ya “Utalii Endelevu kwa Wote”, unaozingatia ustawi wa jamii, utalii wa ndani wa unaotunza mazingira na usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani.
Kwa kuliangalia hilo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka vipaumbele vifuatayo vya Uchumi wa Buluu katika Sekta hii:



