USIMAMIZI WA BAHARI
Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ina mpango jumuishi unaohusisha uratibu wa sekta mbali mbali za Uchumi wa Buluu.
VIPAUMBELE
Kwa kuliangalia hilo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka vipaumbele vifuatayo vya Uchumi wa Buluu katika Sekta hii:
Kuimarisha ushirikiano wa ulinzi katika ngazi zote ili kuhakikisha kuwepo kwa usalama wa bahari
Kuimarisha utayari wa kukabiliana na maafa kwa kuchukua hatua thabiti na za haraka
Kuhamasisha kukuza uelewa, kujenga uwezo wa kiufundi na utaalamu juu ya mpango mkuu wa matumizi ya bahari
Kuandaa mbinu bunifu za upatikanaji wa fedha ili kusaidia kukuza Uchumi wa Buluu katika ngazi zote
Kuimarisha uwezo wa kufanya tafiti na maendeleo ili kuendana na mahitaji ya maendeleo ya siku zijazo
Kuanzisha mfumo wa usimamizi wa taarifa na takwimu za Uchumi wa Buluu unaozingatia maarifa na taasisi za utafiti na habari za Zanzibar na kutumia fursa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
Kuimarisha ushirikiano na mataifa mbalimbali kwa ajili ya kukuza Uchumi wa Buluu na Usimamizi wa Bahari
Kuweka hatua madhubuti za kuzuia VVU/UKIMWI na miripuko katika sekta za Uchumi wa Buluu
Kuimarisha uwezo kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum katika Uchumi wa Buluu
Kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum katika mipango ya Uchumi wa Buluu
Kukuza ubunifu katika sekta za Uchumi wa Buluu kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum
Kuboresha upatikanaji wa soko kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum katika Uchumi wa Buluu



