SEKTA YA UVUVI NA MAZAO YA BAHARINI
Sekta ya Uvuvi ni mojawapo ya nguzo kuu za Uchumi wa Buluu Zanzibar na imeendelea kuwa sekta muhimu sana katika kupunguza umaskini na kuleta maisha bora kwa jamii kupitia uzalishaji wa ajira.
Sekta hii inaajiri watu wanaokisiwa kufikia 78,859 ambao ni sawa na asilimia 8.5 ya nguvu kazi yote ya Zanzibar. Shughuli nyingi za uvuvi hapa Zanzibar ni za uvuvi mdogo ambazo hufanyika katika maji ya kina kidogo cha bahari na kwa kutumia njia za asili. Hata hivyo, mahitaji ya bidhaa za samaki kitaifa na kimataifa yanaongezeka.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia programu zake mbali mbali za maendeleo ikiwemo utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekeleza programu ya uwezeshaji wa wavuvi wadogo wadogo kupitia Mradi wa Ahweni wa UVIKO19 kwa kuwapatia elimu, nyenzo, boti za kisasa na vifaa vya kuvulia Samaki wananchi wote Unguja na Pemba. Programu hii inakwenda sambamba na Programu mbali mbali za wadau wa maendeleo katika Sekta ya Uvuvi ikiwemo UNDP, UN Women, IFAD, Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Ufaransa, JICA, KOICA, n.k.
Halikadhalika, eneo la Ukanda wa Kiuchumi Baharini lina uwezo mkubwa wa kuvutia uwekezaji wa uvuvi kimataifa na hivyo kutoa fursa kubwa kwa wawekezaji wazawa na wa kigeni kwa kuzingatia mabadiliko ya nchi kuelekea Uvuvi wa viwanda.
Sekta ya ufugaji wa viumbe maji Zanzibar inajumuisha ufugaji wa samaki, matango bahari, kaa tope, pweza, chaza, kombe na ukulima wa mwani. Maeneo muhimu ya kuendeleza ufugaji wa viumbe maji ni pamoja na mabwawa, vizimba, na maeneo yenye kujaa maji na kupwa. Sekta hii imeendelea kukuwa kwa kasi kubwa na kuleta mageuzi makubwa ya fursa za Uchumi wa Buluu hapa Zanzibar.
Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kwa hivi sasa inatekeleza vipaumbele mbali mbali ikiwemo:



