Sera Mipango na Utafiti

IDARA YA

SERA MIPANGO NA UTAFITI

Idara ya Mipango Sera na Utafiti ina jukumu la Kuandaa na Kusimamia Utekelezaji wa Sera, Sheria na Mipango ya Wizara. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Dr. Salim Mohamed Hamza
Mkurugenzi Idara ya Sera Mipango na Utafiti

MAJUKUMU YA IDARA YA SERA MIPANGO NA UTAFITI

Kuandaa na kufanya mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni za Wizara
Kusimamia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za Wizara
Kusimamia utekelezaji wa Matamko/Maagizo/Mapendekezo ya Serikali pamoja na kuandaa nyaraka muhimu za Serikali
Kusimamia uandaaji wa Mipango na Bajeti ya Wizara kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi
Kubuni na kuandaa Mapendekezo ya Miradi ya Maendeleo kwa Wizara
Kuandaa viashiria vya matokeo ya utekelezaji wa Mipango ya maendeleo ya Sekta ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi
Kutoa uelewa kwa umma kuhusu Sera, Sheria, Mipango na Mikakati mbalimbali inayousiana na maendeleo ya Sekta ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi
Kuratibu shughuli mtambuka katika sekta ya uchumi buluu na uvuvi
SEHEMU ZA IDARA YA SERA MIPANGO NA UTAFITI

Idara hii inaundwa na Divisheni Kuu nne (4) ambazo ni:

Divisheni ya Maendeleo ya Sera

Divisheni hii inahusika na shughuli za kuandaa, kusimamia nakufuatilia utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za Sekta ya Uchumi Buluu na Uvuvi

Divisheni ya Mipango ya Kisekta na Maendeleo

Divisheni hii inahusika kuandaa na kusimamia utekelezaji Mipango na Bajeti ya Wizara

Divisheni ya Ufuatiliaji na Tathmini

Divisheni hii inahusika na kufuatilia na kufanya tathimini ya utekelezaji wa mipango ya Wizara

Divisheni ya Utafiti

Divisheni hii inahusika na kuratibu tafiti na takwimu kwa Sekta ya Uchumi Buluu na Uvuvi

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.

Melbourne, Australia
(Sat - Thursday)
(10am - 05 pm)
Shopping Cart (0 items)
Translate »