Ugawaji wa Vifaa vya Mwani kwa vikundi 30 Mkoa wa Kaskazini Unguja

  • Mwanzo
  • News
  • Ugawaji wa Vifaa vya Mwani kwa vikundi 30 Mkoa wa Kaskazini Unguja

Wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi zanzibar imekabidhi vifaa vya mwani pamoja na vihori kwa vikundi 30 vya wakulima wa mwani wa mkoa wa kaskazini kwa lengo la kuimarisha na kukuza ongezeko la uzalishaji wa zao hilo zanzibar.

Akizungumza na wakulima hao katika hafla ya ugawaji wa vifaa vya mwani na vihori huko mkokotoni fungurefu katibu mkuu wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi kepten hamad bakar hamad amesema lengo la kugawa vifaa hivyo ni kutimiza ahadi ya mhe. Rais wa zanzibar dkt husein ali hassan mwinyi katika  kuwanyanyua wakulima wa zao la mwani ili kufanya shughuli zao kwa urahisi na kukuza kipato chao na pato la taifa kwa ujumla.

Aidha amesema vifaa hivyo vitakwenda kuwanufaisha wakulima wapatao 600 wa mkoa wa kaskazini unguja waliopo katika vikundi 30 vya ushirika  ambavyo vitawasaidia katika harakati zao za uzalishaji wa zao hilo ambalo kwa sasa limekua ni muhimili mkubwa wa  wauchumi wa zanzibar likishika nafasi ya pili baada ya karafuu

Kepten hamad amesema serikali imefanya jitihada kubwa katika kuboresha uzalishaji wa zao la mwani kwa kutoa elimu, vifaa na soko la uhakika kwa wakulima mbalimbali wa zanzibar kupitia mradi wa uviko, ifad, undp pamoja na maisha bora fondation vilevile raisi mwenyewe alikabidhi takriban boti 500 za mwani kwa unguja na pemba

Amesema mgao wa vifaa hivyo ni muendelezo wa kuimarisha uzalishaji wa zao la mwani kwa wingi wenye kiwango bora utakao ingia katika soko la ushindani la dunia na kuwawezesha wakulima kupata kipato kikubwa kitakacho kidhi mahitaji yao.

Aidha amesema serekali imewahakikishia wakulima soko la uhakika kupitia kampuni ya mwani ya (zasco) hivyo ni vyema wananchi wakachangamkia fursa ya kilimo cha mwani kwani serekali tayari inakamilisha kufunga mitambo katika kiwanda cha kuchakata mwani kiliopo chamanangwe kisiwani pemba kinachotarajiwa kuchakata zaidi ya tani 30 za mwani mkavu lakini pia kitanunua mwani mbichi kutoka kwa wakulima ili kuwapunguzia mlolongo wa kazi.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake wa mwani bi hadia haji makame kwa upande wao wameishukuru serekali ya awamu ya nane na wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi zanzibar kwa msaada huo wa vifaa na vihori, huku akiwataka wakulima wenzake wafanye kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya serekali kama ilivyokusudiwa.

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.

Melbourne, Australia
(Sat - Thursday)
(10am - 05 pm)
Shopping Cart (0 items)
Translate »