Utoaji wa leseni na vibali vya uvuvi

UTALII ENDELEVU

Utalii wetu wa Zanzibar ni utalii wa bahari. Ni utalii unaotegemea uhai na afya ya bahari na rasilmali zake. Hivyo Utalii Endelevu ni ule unaojali hifadhi za maeneo ya bahari, bioanuwai ya bahari, usafi na mazingira safi ya fukwe na bahari zake. Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi inapigania sana Utalii Endelevu wa Zanzibar unaojali mazingira ya bahari pamoja na mila na desturi za watu wa Zanzibar.
Serikali itahakikisha uhifadhi wa mila, desturi na tamaduni za nchi, chini za kaulimbiu ya “Utalii Endelevu kwa Wote”, unaozingatia ustawi wa jamii, utalii wa ndani wa unaotunza mazingira na usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani.

VIPAUMBELE

Kwa kuliangalia hilo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka vipaumbele vifuatayo vya Uchumi wa Buluu katika Sekta hii:

Kukuza matamasha ya kimila na ya kitamaduni na mila za kienyeji katika Uchumi wa Buluu
Kuongeza uwelewa kwa watalii juu ya mila na desturi katika maeneo ya ukanda wa pwani
Kukuza utalii jumuishi unaozingatia uwekezaji na haki za jamii
Kukuza uelewa wa utunzaji wa mazingira na jamii kusimamia rasilimali zao ili kuhakikisha maendeleo endelevu na kuvilinda viumbe vilivyo hatarini kutoweka
Kukuza usimamizi shirikishi wa ulinzi na usalama katika maeneo ya kitalii kupitia Mpango Maalumu wa Matumizi ya Bahari
Kuimarisha mifumo ya kuifanya Zanzibar iendelee kuwa kivutio kikuu cha utalii; na kutekeleza mpango mkuu wa kuijengea uwezo sekta ya utalii Zanzibar

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.

Melbourne, Australia
(Sat - Thursday)
(10am - 05 pm)
Shopping Cart (0 items)
Translate »