Utoaji wa leseni na vibali ya mazao ya baharini

NISHATI MBADALA

Mifumo ya Nishati Mbadala ya baharini inakabiliwa na changamoto ya tafiti na maendeleo, hasa katika vyanzo vya nishati mbadala ya upepo, jua na mawimbi. Uwekezaji wa nishati ya jua na upepo baharini bado haujapata ukondoishwaji wa kitaifa wa hali ya juu hapa Zanzibar. Bila ya kuwepo uwezo wa kutosha wa kiufundi, elimu na mtaji wa kifedha maendeleo ya nishati mbadala yatakuwa ni madogo.

VIPAUMBELE

Kwa kuliangalia hilo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka vipaumbele vifuatayo vya Uchumi wa Buluu katika Sekta hii:

Kukuza tafiti na maendeleo katika mifumo ya nishati mbadala kitaifa na kikanda
Kuimarisha uwekezaji wa ushirikiano wa pamoja kati ya serikali na sekta binafsi katika mifumo ya nishati mbadala baharini
Kuongeza uwezo wa wataalam wa ndani katika kushughulikia nishati mbadala kwa kuwapatia taaluma na uelewa, mafunzo na elimu, na upembuzi yakinifu za kimkakati
Kuimarisha tafiti za nishati mbadala za baharini kwa kuweka mifumo endelevu ya kifedha
Kuendesha mifumo ya kifedha kwa ajili ya uwekezaji wa nishati mbadala endelevu na yenye kusimamiwa vizuri
Kusimamia utekelezaji wa sheria za uhifadhi wa misitu ya mwambao na maeneo muhimu ya makaazi ya viumbe maji
Kujenga uwezo wa kiutendaji na mbinu za uwezeshaji kwa ajili ya kuwanufaisha wazawa
Kuanzisha kitengo maalumu cha nishati mbadala baharini kitakachoshirikisha wadau wa sekta mbalimbali

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.

Melbourne, Australia
(Sat - Thursday)
(10am - 05 pm)
Shopping Cart (0 items)
Translate »