Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia

  • Mwanzo
  • Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia

ZPRA

Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia (ZPRA) imeanzishwa chini ya kifungu cha 7 cha Sheria ya Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia nambari 6 ya mwaka 2016. Mamlaka hii imeanza kazi rasmi mwezi Machi 2017 kufuatia kuteuliwa kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mamlaka. Lengo la kuanzishwa Mamlaka hii ni kukuza, kusimamia na kudhibiti shughuli za Utafutaji, Uendelezaji na Uzalishaji wa rasilimali za Mafuta na Gesi Asilia kwa eneo la Zanzibar kwa kuzingatia Sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia nambari 6 ya mwaka 2016.

Nd. Issa Suleiman Ali
Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi

DIRA

Kuwa mdhibiti bora wa Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia inayochangia kukuza uchumi wa Zanzibar.

DHAMIRA

Kusimamia, kudhibiti na kukuza shughuli za Utafutaji, Uendelezaji na Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwa njia endelevu kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa Zanzibar.

MISINGI MIKUU

Uadilifu na Usiri
Uwajibikaji na Uwazi
Taaluma
Usalama na Uendelevu
Ushirikishwaji wa jamii
Mashirikiano na Ubunifu
MAJUKUMU

Kwa mujibu wa Kifungu cha 8(2) cha Sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia, majukumu ya ZPRA ni kama yafuatayo:

Kufuatilia na kudhibiti shughuli za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia ikijumuisha makisio ya hifadhi na vipimo vya rasilimali zilizozalishwa
Kupitia na kuridhia shughuli ya utafiti iliyopendekezwa na kuwemo katika mpango kazi, mpango wa tathmini na makadirio ya Uzalishaji uliowasilishwa na Kampuni
Kupitia na kuidhinisha bajeti zilizo wasilishwa na Kampuni
Kutathmini mipango ya maendeleo na kutoa mapendekezo kwa Waziri kwa ajili ya kuidhinisha, kurekebishwa au kukataliwa
Kumshauri Waziri katika kutoa na kufuta leseni
Kutathmini hatua za mwisho za Uzalishaji, usitishaji, pamoja na ukomo wa shughuli za Mafuta na Gesi Asilia
Kuandaa ramani ya muongozo itakayoweza kupitiwa mara kwa mara inayoonesha maeneo yenye uwezekano wa Utafutaji na Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia
Kuhakiki gharama za Mafuta au Gesi Asilia za Kampuni
Kuhakikisha kwamba kampuni zinafuata sheria, kanuni, taratibu na masharti ya mkataba
Kufanya au kuwezesha kufanyika utafiti wa awali na kutathmini maeneo muhimu ya Mafuta na Gesi Asilia
Kusimamia mikataba ya Mafuta na Gesi Asilia
Kuhakikisha uvunaji wa hali ya juu wa raslimali za Mafuta na Gesi Asilia
Kuendeleza mipango mizuri inayotekelezeka kwa gharama nafuu
Kuhakikisha matumizi mazuri ya miundo mbinu iliyopo na iliyopangwa
Kuchukua hatua za ulazima kutekeleza matakwa ya leseni au kanuni zozote na kulinda afya na usalama wa wafanyakazi na jamii
Kuhakikisha na kuwezesha ushindani, upatikanaji na matumizi ya miundombinu kwa wengine
Kufuatilia masharti ya waendeshaji na shughuli zao za kibiashara kwa kuhakikisha kwamba ushindani na haki inalindwa
Kuhakikisha washiriki wanafuata Sheria hii na kutoa adhabu kwa wanaopinga au wanaovunja kanuni, amri, taratibu au masharti ya mkataba
Kufanya mambo mengine yote ambayo ni muhimu, ya kuharakisha au ambayo ni muafaka ili kufikia malengo ya Sheria hii
Kushiriki upimaji wa Mafuta na Gesi Asilia na kuruhusu makisio na tathmini ya mrahaba na faida ya Mafuta au Gesi Asilia kwa maslahi ya nchi na itahusika kuidhinisha zoezi hilo
Kuhakikisha uanzishwaji wa Kituo Kikuu cha Mfumo wa Taarifa kwa watu wanaohusika na shughuli za Mafuta na Gesi Asilia, kusimamia taarifa za Mafuta na Gesi Asilia na kutoa taarifa na machapisho ya kila siku kuhusu shughuli za Mafuta na Gesi Asilia
MIRADI

Utafutaji wa rasilimali za Mafuta na Gesi Asilia kwa kitalu cha Pemba - Zanzibar
Uanzishwaji wa kituo kikuu cha kuhifadhia Taarifa za Mafuta na Gesi Asilia
Usafishaji wa Taarifa za zamani za mtetemo kwa eneo la kina kirefu cha maji, eneo la mashariki mwa Zanzibar
MUUNDO

ZPRA imeundwa na Idara 6 ambazo zimegawika katika jumla ya Divisheni 11 kama zinavyoonekana hapo chini: 

Idara ya Utafutaji, Uzalishaji na Uchambuzi wa Kiuchumi

Divisheni ya Utafutaji, Uchambuzi wa Masuala ya Kiuchumi na Taratibu za Utoaji Leseni
Divisheni ya Uendelezaji na Uzalishaji

Idara ya Usimamizi wa Taarifa

Divisheni ya Usimamizi wa Taarifa za Utafutaji na Uzalishaji
Divisheni ya Usalama wa Taarifa

Idara ya Afya, Usalama na Mazingira

Divisheni ya Afya na Usalama
Divisheni ya Mazingira

Idara ya Sheria na Matekelezo

Divisheni ya Uratibu wa Shughuli za Bodi ya Mamlaka na Masuala ya Kesi
Divisheni ya Usimamizi wa Mikataba na Matekelezo

Idara ya Mipango, Fedha na Utawala

Divisheni ya Mipango na Tafiti
Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu
Divisheni ya Fedha

Ofisi ya Pemba
VITENGO

ZPRA ina vitengo 4 vinavyojitegemea ambavyo ni: 

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Kitengo cha Manunuzi na Uondoaji wa Mali chakavu
Kitengo cha Mahusiano ya Umma

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.

Melbourne, Australia
(Sat - Thursday)
(10am - 05 pm)
Shopping Cart (0 items)
Translate »