UENDESHAJI NA UTUMISHI
Idara ya Uendeshaji na Utumishi inahusika na utoaji wa huduma pamoja na kusimamia maslahi ya rasilimali watu ya Wizara, ikiwa ni pamoja na kutunza, kuhuisha na kuhifadhi kumbukumbu za Ofisi. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Nd. Issa Suleiman Ali
Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi
Idara ya Uendeshaji na Utumishi inaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni:-
Divisheni hii inahusika na masuala ya utawala, uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kila siku za Ofisi
Divisheni hii inahusika na masuala ya maendeleo na usimamizi wa rasilimali watu ndani ya Ofisi ikiwemo ajira, mishahara, mafunzo kwa watumishi, upimaji utendaji kazi pamoja na upandishaji vyeo
Divisheni hii itahusika na shughuli za uwekaji wa kumbukumbu na uhifadhi wa nyaraka na kazi mbali mbali za Ofisi



