MAENDELEO NA URATIBU WA UCHUMI WA BULUU
Idara hii inahusika na jukumu la kuratibu utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa Buluu ikijumuisha sekta zilizomo chini ya Wizara lakni pia kushirikiana na Sekta za Uchumi wa Buluu zilizo nje ya Wizara. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Nd. Issa Suleiman Ali
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo na Uratibu wa Uchumi wa Buluu
Idara ya Uratibu wa Maendeleo ya Uchumi wa Buluu itaundwa na Divisheni tano (5) ambazo ni:
Divisheni hii inahusika na kuratibu masuala mtambuka ya Sekta ya Uvuvi
Divisheni hii inahusika na shughuli za uratibu wa masuala ya sekta ya mafuta na Gesi Asilia
Divisheni hii inahusika na uratibu wa Sekta ya Utalii Endelevu
Divisheni hii inahusika na shughuli za kuratibu masuala ya usimamizi wa bahari na sekta za uchumi buluu
Divisheni hii inahusika na kuratibu maendeleo ya miundombinu ya biashara na usafirishaji Baharini



