Uhifadhi na Maeneo ya Baharini

  • Mwanzo
  • Uhifadhi na Maeneo ya Baharini
IDARA YA

UHIFADHI NA MAENEO YA BAHARINI

Idara hii inahusika na shughuli za kusimamia, kuendeleza na kushirikisha jamii katika Uhifadhi wa Maeneo ya Bahari. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Dr. Makame Omar Makame
Mkurugenzi Idara ya Uhifadhi na Maeneo ya Baharini

MAJUKUMU YA IDARA YA UHIFADHI NA MAENEO YA BAHARINI

Kusimamia na kuendeleza maeneo ya hifadhi za bahari
Kuanzisha maeneo mapya ya hifadhi za bahari
Kushirikisha jamii katika Uhifadhi wa maeneo ya bahari
Kufanya tathmini mbali mbali za uendelezaji na Uhifadhi wa maeneo ya bahari
Kutoa uelewa kwa jamii kuhusu Uhifadhi wa bahari na fursa zake za kiuchumi
Kusimamia Doria katika maeneo ya hifadhi za bahari
Kuendeleza maeneo ya urithi yaliyo ndani ya maeneo ya hifadhi za bahari
SEHEMU ZA IDARA YA UHIFADHI NA MAENEO YA BAHARINI

Idara ya Uhifadhi wa Maeneo ya Bahari itaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni:

Divisheni ya Uhifadhi wa mazingira ya bahari, bio-anuwai na rasilimali bahari

Divisheni hii inahusika na kusimamia na kutekeleza mipango ya uhifadhi wa viumbe bahari kama vile mikoko, majani bahari, matumbawe yenye umuhimu wa malisho na kwa ukuwaji wa viumbe vyengine vya baharini pamoja na kuainisha maeneo maalum yenye umuhimu kwa uhifadhi wa rasilimali za bahari

Divisheni ya Uhifadhi shirikishi na maendeleo ya jamii

Divisheni hii inahusika na kutoa mafunzo ya uvuvi, shughuli mbadala za kiuchumi na uhifadhi kwa jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi na wadau mbali mbali wa uhifadhi wa bahari pamoja kufanya jitihada za kuwafikia waliombali (outreach) kuhusiana na mambo mbali mbali yanahusiana na uhifadhi wa maeneo ya bahari

Divisheni ya ulinzi na usimamizi wa sheria (doria)

Divisheni hii inahusika na kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo mbali mbali juu ya uvuvi, utalii na shughuli nyengine kwenye maeneo ya hifadhi na kuendesha doria katika maeneo yote ya hifadhi

Categories

At vero eos et accusamus et iusto odio digni goikussimos ducimus qui to bonfo blanditiis praese. Ntium voluum deleniti atque.

Melbourne, Australia
(Sat - Thursday)
(10am - 05 pm)
Shopping Cart (0 items)
Translate »