UVUVI NA MAENDELEO YA MAZAO YA BAHARINI
Idara hii inahusika na kudhibiti na kuendeleza shughuli za uvuvi endelevu, kilimo cha mwani, na ufugaji wa viumbe maji kama vile Matango Bahari, Kaa Tope, na Samaki. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Nd. Issa Suleiman Ali
Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi
Idara ya Maendeleo ya Uvuvi inaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni:
Divisheni hii inahusika na kuwawezesha na kuwajengea uwezo wavuvi wadogo kwa ajili ya kuimarisha Shughuli za Uvuvi nchini
Divisheni hii inahusika na kusimamia na kuratibu shughuli za ufugaji wa Viumbe vya Baharini pamoja na kuanzisha mashamba ya mfano kwa kushirikiana na jamii katika ukuzaji wa sekta ya Uvuvi
Divisheni hii inahusika na kuratibu shughuli za usarifu na ukuzaji masoko kwa mazao ya Baharini



