DHAMIRA YETU
Kuimarisha usimamizi na matumizi endelevu ya rasilmali za baharí kupitia fursa mbali mbali za uwekezaji katika uchumi wa buluu, ujasiriamali pamoja na uwezeshaji wa wananchi, na kuhakikisha haki na maslahi ya jamii katika fursa hizo.
DIRA YETU
Kuigeuza Zanzibar kuwa kitovu cha maendeleo ya Uchumi wa Buluu katika Eneo la Magharibi ya Bahari ya Hindi.
MALENGO YETU
Kusimamia maendeleo endelevu ya sekta ya Uvuvi na Mazao ya Baharini
Kusaidia na kushajiisha fursa mbali mbali za ubia baina ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi katika Uchumi wa Buluu
Kutekeleza malengo ya uwezeshaji wa waajasiriamali na wananchi kwa ujumla katika Uchumi wa Buluu
Kusimamia utafutaji na uchimbaji wa rasilmali ya mafuta na gesi
Kuendelea na juhudi za utafiti na uwezo katika kutafuta fursa mbali mbali za nishati mbadala
Kupambana na uharibifu na uchafuzi wa mazingira ya baharí na kusimamia hifadhi za maeneo ya baharí
Kusimamia na kuendeleza utafiti wa sekta ya uvuvi na rasimali za baharí
Kuongeza mashirikiano na sekta mbali mbali katika uratibu wa masuala ya diplomasia ya uchumi wa buluu, usimamizi wa baharí na usalama wa baharí
TUNU ZETU
Uwazi
Kujitolea
Ubunifu
Ubora
Umoja
Mashirikiano
VIPAUMBELE VYETU
Uwezeshaji na Uwekezaji katika Uvuvi Endelevu wa Mwambao na Bahari Kuu
Uwezeshaji na Uwekezaji katika Kilimo cha Mwani
Uwezeshaji na Uwekezaji katika Ufugaji wa Viumbe Maji (Matango Bahari, Kaa, Samaki)
Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi
Nishati Mbadala ya Baharini
Ujenzi wa Miundo Mbinu ya Bandari, Masoko, Viwanda, Huduma na Biashara za Uchumi wa Buluu
Utafiti wa Uvuvi, Bahari, Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi Baharini
Uhifadhi wa Maeneo ya Bahari (Matumbawe, Nyasi Bahari, Mikoko na Bioanuwai ya Baharini)
Utalii Endelevu wa Bahari
Usimamizi wa Bahari (Usalama wa Bahari, Kuimarisha Ulinzi wa Bahari na Kupambana na Uvuvi Haramu Usioripotiwa)



